Tuesday , 20th Nov , 2018

Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Bin Zuber Ally amesema jambo la ushoga halikubaliki nchini kwa kuwa ni lenye kumchukiza mno Mwenyezi Mungu na kuwataka viongozi wa dini zote kuungana katika kulikemea.

Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Bin Zuber Ally

Mufti ametoa kauli hiyo leo katika Baraza la Taifa la Maulid lililofanyika wilayani Korogwe Mkoani Tanga ambapo amesema nchi hii ni tukufu na ina watu wenye dini wanaopaswa kukataa ushoga na kuwataka masheikh wa Mikoa kukemea jambo hilo.

Mufi Abubakar Bin Zuber Ally pia amewataka Waislamu nchini kutokubali istilahi zinazowagawa na kuwafanya kila mmoja kupigania jambo leke, akiwaagiza masheikh kuwahimiza waumini wao kutokubali istilahi hizo zenye kuwagawa.

Aidha, Mufti amewataka kujenga uwezo wa kujitegemea kiuchumi kuanzia kwa mtu mmoja mmoja hadi katika ngazi za misikiti na taasisi zake, kwani suala la uchumi limetajwa mara nyingi kwenye Qur'an Tukufu.

Akiongea kwa niaba ya rais Dk. John Magufuli mgeni rasmi Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Selemani Jafo, amempongeza Mufti wa Tanzania kwa umahiri wake na uweledi wa kuwaongoza Waislamuna katika kuimarisha umoja wa Waislamu pamoja na amani nchini.

Jafo amesema ni kweli maadili yetu yamechafuka sana na kuwataka viongozi wa dini wa madhehebu yote nchini kukemea mambo machafu yanayofanywa na watu wachache ili yasije kuiharibia nchi neema iliojaaliwa na Mwenyezi Mungu.