
Ng'ombe anayelishwa na kutunzwa vizuri hutoa kiasi kikubwa cha maziwa na nyama.
Wito huo umetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Titus Kamani pamoja na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa kwa pamoja wakati wakijibu swali la Mhe. Rebecca Mngodo aliyetaka kufahamu serikali inatoa mwongozo gani juu ya kuwapatia chakula watoto mashuleni ikiwa ni pamoja na maziwa.
Aidha, Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI anayeshughulikia elimu ,Mhe. Kasim Majaliwa asema serikali imeshaanza kuteteleza mpango wa chakula na lishe mashuleni kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani WHO, ili kuinua mwamko wa wanafunzi katika shule za msingi nchini.