Theophil Makunga - Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania
Hayo yameelzwa wakati wahariri hao wakiijadili sheria hiyo ambapo wamesema sheria hiyo ni mbaya licha ya kuwa sasa sheria inayolalamikiwa kuwa mbaya zaidi ya magazeti haitatumika tena na kuwataja wanahabari nchini kubuni njia mpya ya kuwatetea wananchi.
Katibu wa Jukwa la Wahariri nchini Tanzania Bw. Neville Meena amesema wangependa kuona mahakama ndicho kinakuwa chombo cha juu cha kutoa haki pindi mwandishi wa habari na chombo cha habari kinapo kinzana na sheria kuliko ilivyo sasa ambapo viongozi wa wizara wamepewa mamlaka makubwa ya maamuzi kuhusu vyombo vya habari.
Wahariri hao wamevitaka vyombo vya habari nchini Tanzania kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria hiyo iliyopitishwa hivi karibuni wakati wakisubiri kutolewa kwa mapendekezo ya kurekebishwa kwa vipengele ambavyo vinalenga kuondoa uhuru wa habari.