Friday , 3rd Jun , 2016

Jumla ya Madawati 776 yamekabidhiwa katika shule 15 za Msingi wilayani Kyela Mkoani Mbeya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Agizo la rais Dokta John Pombe Magufuli la kuhakikisha kila halmashauri inaondokana na changamoto ya uhaba wa Madawati nchini.

Rais Magufuli aliagiza kuwa kabla ya Mwisho wa Mwezi huu halmashauri zote nchini ziwe na Madawati ya Kutosha ambapo katika kutekeleza agizo hilo Wilaya ya Kyela imewashirikisha Wadau mbalimbali kwa ajili ya uchangiaji wa Madawati kwenye shule za Serikali.

Kaimu mkuu wa Wilaya ya Kyela BI, Zainabu Mbusi amesema kuwa pamoja na jitihada za serikali na Wadau kutengeneza Madawati bado halmashauri inakabiliwa na Upungufu wa Madawati  2294 ambayo wanaendelea na juhudi za kutengeneza ili kufikia lengo hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kyela Hanta Mwakifuna amewashukuru Wadau walioachangia Madawati hayo na kwamba nia ya Serikali ni kuboresha Mazingira Bora ya ufundishaji.