
Ice Boy
Akiongea na eNewz Ice Boy amesema anavyoamini yeye ni ngumu sana Tanzania kupata mafanikio kupitia kufanana na Tupac kwa kuwa wananchi na wadau wa sanaa Tanzania hawaitambui faida ya mtu yeyote maarufu hata kama ni staa mkubwa.
Ice amesema ni bora kutengeneza 'brand' yake ili hata ikitokea siku akipata nafasi ya kutoka nje iwe rahisi kutumia hiyo nafasi ya kujitangaza kuhusiana na kufananishwa na Tupac huenda kukamuongezea kitu katika maisha yake lakini kwa sasa anaimba anavyopenda kwani hata akimuiga mwanamuziki huyo hawezi kuongeza mashabiki katika muziki wake.