Akitaja baadhi ya changamoto zinazolikabili zsoko hilo, Mwenyekiti wa soko hilo Bw Suleyman Diwani amesema kuwa soko hilo linakabiliwa na upungufu wa chemba za kuhifadhia maji machafu , barabara za kuingia sokoni hapo kuharibika vibaya, taa kuharibika, uchakavu wa sakafu na miundombinu ya mifereji kuharibika vibaya.
Aidha Bw Diwani amebainisha kuwa wameshawahi kuandika barua mara kadhaa kwa Halimashauri yaManispaa ya kindondoni ili waweze kufanyiwa marekebesho bila ya mafanikio yoyote hali ambayo inaathiri utendaji kazi wa biashara zao.