Monday , 15th Apr , 2019

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kwamba si hoja tu ya Spika kujiuzulu inapaswa kujadiliwa bali maamuzi magumu sana yanapaswa kufanyika ndani ya taifa.

Freeman Mbowe

Akizungumza leo na wanahabari, Mbowe amesema kwamba bunge kwa sasa limekuwa likiendeshwa kama mali binafsi.

Amesema kwamba hata mambo yanayoendelea hivi sasa, Bunge halijamtuma Spika kufanya anayoyafanya, "pamoja na udhaifu wa bunge sisi wabunge hatujamuagiza Spika aende kumuambia CAG kwamba akajieleze kwa Rais, hayakuwa maazimio ya Bunge.

Mbowe amesema kwa sasa wapo kwenye kipindi cha bunge kinachojadili mambo ya msingi kwa mustakabali wa taifa na siyo kujadili maoni ya Watanzania.

Pamoja na hayo ameitaka serikali kuacha siasa za chafu kwa kuwafungia wapinzani huku chama tawala wao wakiendelea kufanya siasa za wazi.