Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo wakiwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mnamo Disemba 30, 2017 eneo la uwanja wa shule ya msingi Mwenge mjini Mbeya.
Jamhuri iliwasilisha mashahdi watano na kielelezo kimoja cha sauti iliyodaiwa kunaswa sauti ambayo yenye maneno yaliyotolewa katika mkutano huo yenye zaidi ya dakika 39 na kuwasilishwa mbele ya Mahakama na Ispekta Joram Magova ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama katika Ofisi ya Upelelezi Mkoani humo.
Upande wa utetezi waliwasilisha mashahidi sita wakiwemo watuhumiwa wenyewe wawili waliokana kutamka maneno ambayo wanadaiwa kuyatoa kinywani mwao.
Kwa mara ya kwanza, washtakiwa Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi "Sugu" na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga walifikishwa Mahakamani Januari 16 na kusomewa mashtaka na Wakili Mkuu wa Serikali Joseph Pande ambapo kesi yao ilikuwa ikosomwa kwa muendelezo mpaka ilipofikia Februari 09, 2018 ambapo waliachiwa kwa dhamana ya milioni tano kwa kila mmoja.




