Thursday , 13th Oct , 2016

Serikali ya Tanzania imetakiwa kudhibiti uzalishaji, usafirishaji na matumizi ya kemikáli za sumu ili kuwalinda wananchi wake dhidi ya madhara ya kemikáli hízó hasa wale wanaotumia dawa za meno zenye kemikali hizo kwa ajili ya matibabu ya meno.

Rais wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Meno Tanzania Dkt. Lorna Carnero

Akiongea leó jijini Dar es Salaam, katika maadhimisho ya síkú ya Afrika ya kutibu meno bila kutumia dawa yenye madini ya Zebaki duniani, Afisa Programú wa Taasisi ya AGENDA, Bw. Silvani Mnganya amesema ni vyema serikali ikadhibiti matumizi ya tiba kwa madini hayo ambayo hupelekea magonjwa ya saratani, kupöteza kumbukumbu na ubongo kushindwa kufanya kazi vizuri na kuharibu mfumo wa hewa na wa uzazi.

Afisa huyo amesema, Bara la Afrika hutumia kemikali za sumu kwa silimia 10 tu tofauti na mataifa yaliyoendelea lakini madhara ya kemikali hizo ni makubwa zaidi hivyo mkakati wa pamoja wa bara hilo kudhibiti madhara yake umeadhimishwa kote barani Afrika hii leo.

Nchini Tanzania kemikali ya Zebaki hutumika kwenye tiba ya kuziba meno, uzalishaji wa viwandani na katika machimbo ya madini, lakini Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto nchini inaanda mkakati wa kudhibiti kemikali hizo hasa Zebaki ambayo athari zake ni nyingi kiafya kwa mujibu wa Afisa Afya Mkuu wa Wizara hiyo Bi Anne Sekiete.

Naye Rais wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Meno Tanzania Dkt. Lorna Carnero amesema kukwepa matumizi ya zebaki kwenye matibabu ya jino ni ngumu lakini serikali ihakikishe inaingiza dawa zisizo na madhara kiafya na kuasa jamii kupima meno mara kwa mara kuepuka madhara hayo.