
Shirika la Reli nchiniTanzania TRL linatarajia kuanza kutoa huduma ya uuzaji wa tiketi kwa njia ya kielektroniki lengo likiwa ni kuwawezesha wananchi kuweza kurahisisha ununuaji wa tiketi hizo na kupunguza usumbufu kwa abiria.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, alipokuwa akijibu swali la nyongeza lililohusu wizara yake na kutaja maeneo ambayo mfumo huo utaanza kufanya kazi kuwa ni pamoja na Mpanda mpaka Tabora na Kigoma mpaka Tabora.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Edwin Ngonyani, amesema kuwa kwa hivi sasa uuzaji wa tiketi katika maeneo yenye uhitaji mkubwa wa huduma hiyo maeneo ya Kigoma yanachangamoto kubwa hasa baada ya kuwepo kwa tabia ya ulanguzi wa tiketi hivyo ili kuthibiti tabia hiyo shirika liliamua kuuza tiketi siku za safari na kwa kutumia vitambulisho hali iliyopelekea baadhi ya abiria kulala stesheni ili kuwahi tiketi hizo.
Aidha, shirikala reli linamikakati ya kuongeza idadi ya treni zitakazosaidia kupunguza msongamano wa abiria na kwa utaratibu wa kulipia kielektroniki watakomesha kabisa changamoto za upatikanaji wa tiketi.