
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi, Nicolas Mgaya
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi, Nicolas Mgaya amesema wamebaini wageni wengi wanfanya kazi kwa kujificha katika viwanda mbalimbali nchini kwa kufanya kazi mchana na kutoka usiku.
Mgaya amesema ili fursa za ajira ziongezeke nchini serikali haina budi kupita kiwanda kwa kiwanda nyumba kwa nyumba ili kuwabaini wafanyakazi raia wa Kigeni wanaofanya kazi kinyume cha sheria.
Aidha Mgaya ameongeza kuwa kwa sekta nyingi za uzalishaji ikiwemo na mahoteli zimevamia na rais wa kigeni kutoka nchi jirani na kufanya shughuli ambazo hata watanzania wengine wa kawaida wana uwezo wa kuzifanya.