Sunday , 16th Oct , 2016

Uhaba wa damu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili umepungua kwa kiasi, ambapo kwa mujibu wa Mhamasishaji Mkuu wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama hospitalini hapo Bw. Khamis Kubiga, mahitaji ya damu hivi sasa ni wastani wa chupa 160 kwa siku

Kubiga amesema hayo katika hafla ya uchangiaji damu iliyoendeshwa na klabu ya mazoezi ya viungo ya 'Kawe Jogging', ambapo viongozi wake akiwemo mlezi wa klabu hiyo diwani wa Kawe Muta Lwakatare, wametoa wito kwa wana Kawe kujenga utamaduni wa kujitolea kuchangia damu.

Kwa mujibu wa Bw. Kubiga suala la uchangiaji damu ni endelevu kwani suala la uhitaji wa damu ni la dharura ambalo wahitaji hawawezi kujiandaa, hivyo jamii imeombwa kuendelea kuchangia ili kuokoa maisha ya wagonjwa.