Wednesday , 6th Jan , 2016

Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamadi Masauni ameitaka idara ya uhamiaji nchini kuwasaka, kuwakamata, kuwashtaki na kuwarudisha makwao raia wote wa kigeni wanaoishi bila vibali halali vya kuishi na kufanya kazi hapa nchini,

Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamadi Masauni

Naibu waziri Masauni amesema kuwa wageni wote wanaonyanyasa watanzania katika makampuni yao washughulikiwe haraka na wale wanaofanya kazi zinazoweza kufanywa na wazawa waondolewe nchini ili watanzania wapate hizo ajira.

Aidha masauni ameongeza kuwa idara ya uhamiaji itaanzisha mahakama yake ya kijeshi ili maafisa wasio waaminifu na wala rushwa washughulikiwe haraka ili kuleta uadilifu katika sekta hiyo,

Wakati huo huo Kamishina wa uhamiaji wa mkoa wa Dar es Salaam, John Msumule amesema wanatarajia kukamata wageni 350 katika kampeni inayoanza leo japo kuna changamoto ya uchache wa watumishi pamoja na vitendea kazi kama magari na fedha za kuwasarifisha wale watakaotakiwa kurudishwa nchini mwao.