Tuesday , 12th Aug , 2014

Vitendo vya ukatili kwa watoto vimeendelea kujitokeza jijini Arusha baada ya kuripotiwa kwa Mtoto Fanoria Lembris kupigwa kwa panga na kaka yake kwa madai ya kuiba pesa kiasi cha elfu thelathin katika eneo la Sombetini.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Sophia Simba.

Mtoto huyo ambaye analelewa na mama yake mkubwa akitokea mkoani Iringa aliletwa kwa madai ya kusomeshwa jambo ambalo limekuwa kinyume kwa kuwa amekuwa akinyanyasika kwa kupigwa na kusababishiwa majeraha mara kwa mara.

Nao, baadhi ya wakazi wa eneo la Sombetini wamelaani kitendo hicho huku wakiwataka wazazi waliopo vijijini kuacha tabia ya kuwaamini watu na kuwapa watoto wao jambo ambalo baadaye huwa mateso kwao.

Baadhi ya wazazi kutoka maeneo ya vijijini, wamekuwa na tabia ya kukubali kuwatoa watoto wao na kwenda kufanya kazi za ndani katika maeneo mbali na kwao hali inayowaweka watoto hao katika hatari mbalimbali ikiwemo matukio ya unyanyasaji wa kijinsia.