Mkurugenzi Mtendaji wa Progress Center Bi Rose Urio.
Mkurugenzi wa Progress Center Bi Rose Urio amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha akisisitiza kuwa muitikio duni kwa washiriki bado ni jambo linaloonesha dhahiri kuwa wamiliki bado wanahitaji elimu zaidi katika uwekezaji huo.
Bi. Urio amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuimarisha sekta hiyo ambayo inaenda sambamba na utalii ili kuongeza pato kwa wamiliki wa hoteli lakini pia kuongeza pato la taifa kupitia kodi
Kwa upande wake mmoja wa mameneja wa Hotel Mkoani humo Neema Gervas amesema umuhimu wa mafunzo hayo ni pamoja na kuwawezesha kutoa huduma bora ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.