
Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii nchini Tanzania, Rabikira Mushi amesema kwamba watoto wengi nchini wanalelewa na wazee kutokana na kufariki kwa wazazi wa watoto hao kutokana na ugonjwa wa Ukimwi ambao umeuwa vijana wengi ambao tayari walikuwa na watoto.
Kaimu Kamishna huyo ametoa kauli hiyo leo katika mahojiani na East Africa Radio katika hafla ya kukabidhi zawadi za pasaka zilizotolewa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye vituo vya wazee na watoto yatima nchi kote.
Mushi ameeleza changamoto nyingine kubwa za ustawi wa jamii nchini kuwa ni pamoja na uchumi duni wa familia, mafarakano ya familia kwa wazazi kunywa pombe kupita kiasi pamoja na kukosekana kwa desturi ya kujaliana hasa maeneo ya mijini.