Wednesday , 7th Dec , 2016

Kukosekana kwa Nishati ya umeme kwenye kituo cha afya katika kata ya Ulaya Wilayani Kilosa mkoani Morogoro, kumepelekea wananchi wa kata hiyo kukosa huduma muhimu za upasuaji hasa kwa mama wajazito wakati wa kujifungua hivyo kutumia vibatari

 

Hali hiyo imekuwa kero ya muda mrefu kwa wananchi hao, ambapo kituo hicho cha afya ndicho pekee kwenye kata hiyo, na kinahudumia wagonjwa zaidi ya mia mbili kwa siku, huku kikiwa kinategemea nishati ya umeme wa jua ambao hautoshelezi mahitaji ya kituo hicho.

Hata hivyo Kaimu Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Ulaya ameeleza bayana changamoto iliyopo kwa kukosa huduma ya nishati ya umeme, huku Naibu waziri wa Nishati na Madini Dakta Medard Kalemani akiahidi kutatua changamoto hiyo. 

Diwani wa kata ya Ulaya Raymond Chengula (Wa kwanza kushoto)

Katika kuhakikisha wananchi wa kata hiyo wanaondokana na adha ya kutembea umbali mrefu wa kwenda kulipia gharama za kuunganishwa umeme wa REA Naibu Waziri amemwagiza meneja Tanesco mkoa wa Morogoro kuhakikisha panafunguliwa ofisi katika kata hiyo.