
Mkurugenzi mkuu wa TMA Dakta Agnes Kijazi.
Mkurugenzi mkuu wa TMA Dakta Agnes Kijazi ametoa kauli hiyo kwa vyombo vya habari kuelekea maadhimisho ya siku ya hali ya hewa duiani hapo kesho.
Katika taarifa hiyo Dakta Kijazi amebainisha kuwa vijana ni chachu ya kuwa mstari wa mbele katika kufuatilia taarifa za hali ya hewa zitolewazo na mamlaka hiyo ili kuwa tayari kutoa elimu kwa watu wengine juu ya madhara yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.