Thursday , 24th Mar , 2016

Wananchi kutoka kata tatu zinazozunguka Mgodi wa Geita (GGM), wameanza kunufaika na mradi wa kilimo cha kisasa baada ya kupewa mafunzo ya ulimaji wa kisasa kutoaka chuo cha utafiti wa Kilimo Dakawa kilichopo mkoani Morogoro.

Wanakijiji pembezoni mwa Mgodi wa GGM wakiwa katika shughuli za Kilimo.

Imebanishwa kuwa kutokana na mradi huo imepunguza wimbi la vijana kufanya uharibifu katika maeneo ya Mgodi wa dhahabu wa Geita,ambao unazungukwa na kata za Mugusu, Mugulula, na Nyamilolwa Wiyani Geita.

Akizungumza na wakulima hao Afisa utafiti kutoka chuo cha Utafiti cha Dakawa, Rajabu Kangile, amewataka wakulima wa maeneo hayo kutumia aina ya mbegu ua mpunga aina ya Saro ambayo inahimili hali ya hewa ya Ukanda wa maziwa makuu.

Baadhi ya wakulima wamesema kuwa elimu waliyopewa ya Kilimo cha Kisasa imeweza kuwanufaisha zaidi kuliko hapo awali na kusema kuwa wanawake wengi wameweza kujikomboa kiuchumi kutokana na kilimo hicho.

Wakulima hao wamesema kuwa kwa kuwa kilimo kinaoneka kuwa ni mkombozi wa vijana wengi hivyo mafunzo zaidi yanahitajika kwa vijana hao kutokana na ukweli kwamba shughuli ya kilimo ni ngumu.