
Mbunge wa jimbo la Mikumi Mhe.Joseph Haule
East Africa Redio imeshuhudi mashamba na nyumba hizo zikiwa zimeanguka kabisa na nyingine kubomoka huku waathirika wa mafuriko hayo wakiomba msaada waharaka ikiwemo chakula, hifadhi ya muda pamoja na mbegu za mahindi za muda mfupi ili wapande upya ili kuwaepusha na baa la njaa.
Nao viongozi wa Serikali ya Kijiji na Kata wameomba msaada wa dharula kuwasaidia wananchi hao huku wakieleza sababu ya mafuriko hayo ni kutokana na Mto Miyombo kubadili uelekeo na kumwaga maji kwenye makazi na mashamba ya wananchi na kwamba jitihada za kurudisha tuta la Mto huo zinahitajika ili kuzuia maafa kwa wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Mikumi Mhe.Joseph Haule amefika katika kijiji hicho ambapo amesema anafanya jitihada za haraka kuhakikisha wananchi wanapata msaada wa hifadhi ya muda, chakula pamoja na mbegu na kuhusu tuta amesema kazi hiyo itaanza mapema mvua zitakapopunga.