
Hali hiyo imetokea baada ya Naibu Spika Tulia Mwansasu kumtaka katibu wa Bunge kuarifu bunge ratiba inayoendelea, ambapo katibu wa Bunge alibainisha kwamba kazi ya ratiba ya inaonesha kwamba ni kuchangia hotuba ya Rais aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge.
Baada ya hapo wabunge wa upinzani waliomba miongozo kutoka kwa Naibu Spika, ambapo Naibu spika amemruhusu mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko ambapo Mbunge huyo ameuliza swali kuhusu mapungufu yaliyojitokeza kwa elimu bure kwa wanafunzi kutozwa michango ya chakula katika jimbo lake.
Naibu wa spika akitoa majibu ya muongozo huo ambapo amesema kwamba serikali inatambua matatizo yanayojitokeza na inayafanyia kazi.
Jambo hilo limewakasirisha wabunge wa upinzani na kuzidi kuomba miongozo ambapo Naibu Spika amewakataza na kuruhusu ratiba iliyo mbele ya bunge kuendelea, hali ambayo imewafanya wabunge wa upinzani kutoka nje.
Hata hivyo wabunge wa upinzani baada ya kutolewa nje bunge siku ya jana, wameendelea kushinikiza kwamba hawawezi kukubali serikali kuendesha mikutano ya Bunge bila kuonesha live kwa kisingizio cha fedha kukosekana.