
Wakizungumza na mwakilishi mpya wa serikali ya DRC hapa nchini Balozi Jean Pierre Mutamba; wafanyabiashara hao wakiongozwa na Rais wao Bw. Mutendi Kaboudu wametaja baadhi ya vikwazo hivyo kuwa ni urasimu katika mfumo wa kupata vibali vya kupitisha mizigo pamoja na utaratibu usioridhisha kwenye mfumo wa uondoaji mizigo kwa njia ya TEHAMA..
Kwa upande wake, balozi Mutamba amewaahidi wafanyabiashara hao kuwa atawasiliana na mamlaka za hapa nchini kuona jinsi ya kushughulikia malalamiko yao, lakini akawaonya kuwa wahakikishe wanafanya biashara zao kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi na si vinginevyo.