Monday , 28th Mar , 2016

Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo jijini Dar es salaam wamesema kuwa hali ya biashara kwa msimu

Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo jijini Dar es salaam wamesema kuwa hali ya biashara kwa msimu huu wa sikukuu ya Pasaka ni ngumu ukilinganisha na misimu ya sikukuu zilizopita kwani hamna wateja wa kutosha na bidhaa nyingi zimebaki kama zilivyokuja sokoni .

Wakiongea na EATV wafanya biashara hao wamesema kuwa wanahusisha hali ya biashara ilivyo sasa na mabadiliko ya uongozi yaliyopelekea mzunguko wa pesa kupungua mikononi mwa watu hivyo watu wengi kushindwa kufanya manunuzi.

Wafanyabiashara wengine wanahusisha hali hiyo na mabadiliko ya utaratibu katika maeneo ya Bandari kwani kwa sasa kumekuwa na ucheleweshaji wa kutoa Mizigio bandarini hasa kutokana na taratibu za utoaji mizigo kufuatwa kikamilifu na kupelekea baadhi ya mizigo kukwama bandarini mpaka baada ya sikukuu..