
Wakulima wa korosho wakikusanya mazao mara baada ya kuvuna.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliowakutanisha wananchi wa vijiji vya Sengenya na Matimbeni, wamedai kuwa agizo hilo linawafaa wakulima wanaokusanya kiasi kikubwa cha korosho ambao fedha zao zinapaswa kulipwa kwa njia ya benki
Diwani wa kata ya Sengenya, Fatma Chisanga, ameshauri wanaopaswa kulipwa kupitia benki ni wale wanaokusanya zaidi ya kilo 500 na kutoa tahadhari kwamba agizo hilo linaweza kupelekea wakulima wadogo kushawishika kuuza kwa wanunuzi holela maarufu Kangomba.
Afisa mtendaji wa kijiji hicho, Athuman Makochela, amewaonya wakulima kutothubutu kuuza kwa wanunuzi wa Kangomba na kwamba watakaofanya hivyo serikali haitasita kuwachukulia hatua.