Monday , 26th Nov , 2018

Imebainika kwamba watu waliokuwa kwenye boti ambayo ilizama ziwa Victoria nchini Uganda na kusababisha idadi ya vifo 31 mpaka sasa, walikuwa wakila bata hali iliyopelekea kutokumbuka usalama wa maisha yao.

Boti hiyo ambayo ilikuwa imebeba watu takriban 100 iilikuwa imekusanya watu mbalimbli maarufu wa nchini humo wakiwemo wanachuo na marafiki zao, ambao walikuwa wakiparty na kunywa pombe kwa wingi.

Mmoja wa manusura wa ajali hiyo aliyejulikana kwa jina la Shamira Nseleko, amesimulia kuwa  wengi wao walikuwa wamelewa kutokana na pombe walizokunywa, hivyo hata zilipoanza kutokea dalili za ajali hawakujali sana wakiamini ni kawaida.

Boti ilikuwa ikipoteza muelekeo, lakini tulidhani ni hali ya kawaida, kijana mmoja alituambia tuidhibiti, lakini kumbuka alikuwa anaongea na watu ambao walikuwa wamelewa, ghafla tukaona spika inaanguka, tukaanza kuweka balance kwa kwenda upande ambao ulikuwa unainuka, huku tukiamini ni kitu cha kawaida, ghafala ikazima”, alisema shuhuda huyo Shamira Nseleko.

Msanii Iryn Namubiru ni mmoja wa wahanga wa ajali hiyo ambaye aliokolewa na mvuvi, anasema kwamba anashukuru Mungu amenusurika lakini tukio hilo bado linamuumiza nafsi, kwa kuona rafiki zake wengi wamekufa.

Pia kwenye ajali hiyo kulikuwa na Mwana Mfalme wa Buganda, David Wasajja, ambaye naye alifanikiwa kuokolewa na mvuvi.

Vyombo vya usalama nchini Uganda vimethibitisha kuwa mpaka sasa waliothibitika kufariki ni watu 31, waliokolewa 26, na wengine bado hawajapatikana hivyo wanaendelea kutafutwa.

Kutokana na ajali hiyo Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda ametoa pole kwa familia na wananchi wa Uganda, na kutaka kufanyika ukaguzi wa vyombo vya majini, na kuangalia kama vimesajiliwa.

Msanii Iryn Namubiru