
Wito huo aliutoa jana Jijini Arusha, wakati wa semina ya siku tano iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), iliyoshirikisha askari Polisi 30 toka Wilaya sita za Mkoa wa Arusha.
Amesema lengo la kutoa mafunzo hayo kwa Polisi ili kuboresha utendaji kazi wao na waathirika wa matukio ya ukatili huo, kwa ajili ya kuwaweka huru zaidi waathirika wa ukatili wa kijinsia.
Chialo amesema matukio ya ukatili wa kijinsia Tanzania yanazidi kuongezeka na hiyo inatokana na mwamko mkubwa uliopo kwenye jamii sababu ya mafunzo yanayotolewa na mtandao huo kwa ushirikiano wa Dawati hilo.
Ametoa mfano wa matukio waliopokea nchi nzima kwenye dawati hizo mwaka 2013 ni 8,270 kati yao wakubwa walikuwa 3,081 na watoto 5,189 na mwaka huu 2014 wamepokea 6,511, wakubwa 5,868 na watoto 643.
Amesema takwimu hizo inaoonyesha kwa mwaka huu, watapokea matukio mengi kwa sababu ndiyo mwaka umeanza na tayari wamepokea matukio hayo na kati ya matukio hayo kesi za kubaka zinaoongoza na kufuatiwa na utelekezaji wa familia.
Kwa upande wake Afisa Mipango wa Shirika lisilo la kiserikali la kijinsia Tanzania, TGNP, Donald Donald, amesema wameshatoa mafunzo hayo mikoa ya Mwanza, Singida, Mara na Manyara na wametoa Kompyuta sita na Printer sita kwa Arusha na Manyara, lengo kuboresha madawati hayo nchi nzima.