
Mwalimu wa Idara ya Sanaa Bunifu Katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Safina Kimbokota amesema kuwa wasanii wa sanaa banifu wanatoa mchango mkubwa sana kwenye jamii na kuitangaza nchi ya Tanzania kimataifa hivyo ni jukumu la nchi kuwathamini kwa kazi wanazozifanya.
Bi. Sakina ameitoa kauli hiyo kwenye mahojiano maalum na East Afrika Radio na kubainisha kuwa wizara husika mara nyingine hawaoni juhudi zinazofanywa na kundi hilo na kufikia hatua kushindwa kugharamia ushiriki wao kimataifa hali inayorudisha nyuma sanaa yao.
Aidha. Bi. Sakina ametoa wito kwa serikali kuwapa kipaumbele wasanii wa ndani kwa kuwapa fursa ya kuonesha kazi wanazozifanya na kutumika katika kutafuta suluhisho la matatizo kwa kutumia sanaa.