
Bi Lusimbi ameyasema hayo katika mahojiano maalum na East Africa Radio ambapo amesema kuwa sambamba na kuwawezesha wanawake mbalimbali nchini pia wamewajumuisha na vijana kutoka mikoa mbalimbali ili kuhakikisha wanawainua kiuchumi na kuacha utegemezi wa kipato.
Amesema wanashirikiana na mashirika mbalimbali duniani katika kutoa ruzuku ambayo itasaidia kuwawezesha kufanya biashara mbalimbali ambazo wana lengo la kuzifanya kinamama hao na kujikwamua zaidi ili kufikia kipato cha kati.
Kwa upande wake mwalimu wa wajasiriamali hao Rose Julius amekemea tabia ya wanawake ambao wanaamini hawawezi kufanya mabadiliko bila kuwa na nguvu ya zaidi na kuwataka wajiamini katika utekelezaji wa majukumu yao.
Aidha wameiomba serikali kurudisha kwa haraka swala la mchakato wa katiba mpya ili kubadilisha baadhi ya mitazamo ambayo imezoeleka kwa wanawake na jamii kwa ujumla.
