Sunday , 16th Mar , 2014

Kanisa la Waadventista wa Sabato wawataka Watanzania kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wenye uhitaji

Askofu mkuu wa kanisa la Waadventista Wasabato nchini Tanzania jimbo la Mashariki na Pwani, mchungaji Mark Malekana, ameiomba jamii ya Watanzania kujitolea kuchangia damu kwa lengo la kuokoa maisha ya wale wenye uhitaji mkubwa.

Askofu Malekana ametoa wito huo jijini Dar es Salaam wakati waumini wa kanisa hilo walipoamua kujitolea kuchangia damu kupitia mpango wa damu salama Tanzania, kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya matendo ya huruma ambayo kanisa hilo huadhimisha mwezi Machi kila mwaka.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa mpango wa taifa wa damu salama Bw. Rajab Mwenda amesema sasa hivi kuna upungufu wa damu unaokadiriwa kufikia asilimia 72 ya mahitaji halisi, ambayo ni chupa laki nne na elfu hamsini kwa mwaka.