Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Watishia kuchana muswada wa vyama ukienda bungeni

Friday , 14th Dec , 2018

Muungano wa Baraza la Umoja wa Vyama vya Upinzani nchini wamelalalamikia muswada wa sheria ya mabadiliko ya vyama vya siasa nchini kwa kile walichokidai kuwa muswada huo umelenga kuwabana vijana hao.

Wakizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam vijana hao wametishia kuuchana muswada huo pindi utakapofikishwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa.

Aidha katika Mkutano vijana hao kutoka vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR - Mageuzi na CHAUMA  waliingia kwenye mkutano huo kwa kile walichoashiria kuwa ni majonzi waliyokuwa nayo juu ya muswada huo.

"Leo hii sisi tumevaa nguo nyeusi, hatuoni 'future' sasa basi vijana tunataka umoja tunapinga ili tuendeleea kuwa wamoja, Taasisi zote za vijana nchi hii kwa mara ya kwanza tutatangaza safari na tutauchana muswada ukiwa unataka kuingia bungeni," amesema Likapo Bakari ambaye ni Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT wazalendo.

"Muswada unampa mamlaka msajili kutoka kuwa mlezi wa vyama vya siasa, hadi kuwa  mdhibiti wa vyama vya siasa, hivyo basi baada ya kuutafakari kwa kina muswada huu, tumeona ndoto za vijana ziko hatarini kufa kabisa na hali ya vijana itakuwa mbaya zaidi kuliko hata ilivyo sasa, hatukubaliani nao hata kidogo," amesema Patric Ole Sosopi, Mwenyekiti BAVICHA.

Aidha Mwenyekiti wa JUVI-CUF taifa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mchinga mkoani Lindi, Hamidu Jabali, amesema kuwa mchakato wa vikao vya upembuzi wa muswada huo vinaendelea baada ya kila chama kutoa wajumbe wanne watakoingia katika timu waliyoiita ya ufundi ambapo watatoa tamko rasmi baada ya kumaliza mchakato huo.

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya