Friday , 11th Nov , 2016

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema watoto 400 ulimwenguni hufariki dunia kila siku kutokana na surua licha ya kuwepo kwa vifaa na utaalam wa kukabili ugonjwa huo.

Watoto wakipatiwa chanjo

 

Kupitia ripoti mpya , UNICEF imesema licha ya kupungua kwa asilimia 79 kwa vifo vitokanavyo na surua kati ya mwaka 2,000 na 2015, bado watoto wanapata ugonjwa huo wenye chanjo.

UNICEF kupitia ripoti yake hiyo, imesema licha ya kupungua kwa vifo vitokanavyo na surua kati ya mwaka 2000 na 2015, bado watoto wanapata ugonjwa huo wenye chanjo, sababu ikitajwa kuwa ni ukosefu wa utashi wa kisiasa wa kuwezesha kila mtoto kupata chanjo popote alipo.

Dkt. Richard Keezala ni mshauri mwandamizi wa masuala ya afya, UNICEF anasema kile wanachofanya kukwamua hali hiyo ni kufanya kazi na serikali katika ngazi ya kitaifa na hata kimkoa na kusaka kutengwa kwa bajeti kutoka serikali kuu au serikali za mkoa ili watambue suala la chanjo kwa watoto