
Mkurugenzi wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini, Bi. Hellen Kijo-Bisimba.
Amesemana watoto hao wanakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo kunyimwa fursa mbalimbali za kimaendeleo na elimu pamoja na ukatili wa kijinsia dhidi yao.
Akizungumza na East Africa Radio hii leo, Bi. Kijo-Bisimba amesema kuwa mtoto wa kike anaendele kukosa fursa, kubaguliwa na kufanyiwa ukatili, ikiwemo kupewa mimba wakiwa shuleni, kubakwa vitendo ambavyo vinafanywa na ndugu wa karibu hali inayoashiria uvunjifu wa haki za binadamu dhidi yao.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa tatizo kubwa linalosababisha unyanyasaji wa watoto kike kuendelea na kutokana na mifumo iliyopo nchini ikiwa ni pamoja na jamii kutokuwa na imani na watoto wa kike kama wanaweza kuwa chachu ya maendeleo kupitia fursa mbalimbali watakazopatiwa.
Bi. Kijo Bisimba amesema kuwa elimu iliyotolewa bado haijasaidia kwa kiasi kikubwa kuwakomboa watoto wa kike duniani kote hali hivyo serikali hazina budi kuongeza juhudi katika kutoa elimu juu ya haki za mtoto wa kike ili kumaliza ukatili dhidi yao hali inayowafanya washindwe kupiga hatua za kimaendeleo.
Ameongeza kuwa jamii inatakiwa kuacha kuwakuza watoto kibaguzi kwa kuwapa kipaumbele watoto wa kiume kupata elimu huku watoto wa kike wakibaguliwa wakionekana mwisho wao ni kuolewa na hakuna shughuli yoyote ya kuitumikia jamii ambayo wanaiweza.