
Ban Ki-moon
Ban amesema hayo katika ujumbe wake wa siku ya mtoto wa kike hii leo, maudhui yakiwa ni maendeleo ya mtoto wa kike ni maendeleo ya SDGs, kipi muhimu kwa mtoto wa kike.
Amesema Umoja wa Mataifa umeazimia kumaliza ubaguzi na ghasia dhidi ya mtoto wa kike, sambamba na mila potofu kama vile ndoa katika umri mdogo.
Kwa mantiki hiyo amesema ahadi imeshatolewa hakuna mtu atakayeachwa nyuma kwenye malengo hayo, wakati huu ambapo mara nyingi vijijini na hata kwenye kambi za wakimbizi watoto wa kike husahaulika.
Amesema kuwekeza kwa mtoto wa kike ni jambo la msingi kufanya na bora vile vile, hivyo ametaka kila mtu kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha watoto wote wa kike wanajumuishwa kwani kila mtoto wa kike ana umuhimu.