
Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya El Niño na mabadiliko ya tabianchi, Balozi Macharia Kamau.
Amesema kati ya watu milioni 1.5 na milioni 2.3 wanateseka na ukame ulioletwa na El Niño nchini.
Balozi Kamau ambaye yuko ziarani kwenye ukanda wa Kusini mwa Afrika, amesema matumaini yake ni kujionea mwenyewe hali ilivyo, kuongea na viongozi kudhihirisha mshikamano wa jumuiya ya kimataifa na vile vile kuongeza uelewa wa changamoto zinazoikumba Msumbiji.
Wananchi nchini Msumbiji walioathirika na ukame
Wakati wa ziara hiyo nchini Msumbiji, Balozi Macharia amekuwa na mazungumzo na Rais Filipe Nyusi ambapo wamekubaliana kuwa Umoja wa Mataifa na nchi za kigeni zijitahidi kuisaidia Msumbiji.
Amesema janga hilo si geni nchini Msumbiji, lakini dhoruba yake inazidi kuwa kubwa zaidi kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na kuisihi nchi hiyo kuondokana na utegemezi wa nje, kwa kuweka mikakati endelevu.