
Taarifa hiyo imetolewa leo kwa vyombo vya habari kwenye barua iliyoandikwa na Naibu Mkurugenzi wa TAKUKURU Bregadia Jenerali John Mbungo, ambayo imeweka wazi juu ya kupata kwa taarifa aliyoitoa Zitto Kabwe juu ya uwepo wa rushwa kwenye makampuni ya chuma.
Baada ya barua hiyo kumfikia mwenyewe Zitto Kabwe, ametumia ukurasa wake wa twitter kuijibu na kusema ataitikia wito huo, huku akiwataka TAKUKURU kuweka wazi taarifa zote atakazowapa na kuzifanyia uchunguzi.
Nitakwenda kwa roho nyeupe kabisa. Wawe tayari kusema hadharani nitakayoyasema na kuchunguza nitakayowaambia. Hujuma dhidi ya Mradi wa kimkakati wa #MchuchumaNaLiganga hazivumiliki na zinatoka juu kabisa. Poleni wana #KaziNabata jamaa wamenikurupua huko. Narudi batani. Ciao pic.twitter.com/ciRoovBmc2
— Zitto Kabwe Ruyagwa (@zittokabwe) December 1, 2018