
Tabla
Akizungumza na EATV, Tabla amesema mpango wake ni kutoa albam ya kwanza akiwa na umri wa miaka 35 mwaka 2021 na kwamba hiyo ndiyo itakuwa albam pekee katika maisha yake.
"Albam yangu ya kwanza itatoka 2021 nitakapo timiza miaka 35 panapo majaliwa ya uzima. Na itakuwa ni moja tu katika maisha yangu ya muziki, albam hiyo itakuwa na track 100. Mwezi wa tano nitaachia single nyingine baada ya hii.. kwa mwaka huu nitatoa track 3 tu". Amesema Tabla.
Kwa upande mwingine msanii huyo ambaye amepania kubadilisha upepo wa bongo fleva kwa kutoa kazi bora bila kuimba maudhui ya mapenzi, amesema kwa sasa muziki umekuwa wa gharama zaidi ikilinganishwa na miaka ya nyuma, kwa maana ya gharama za kurekodi, kutengeza video na kujitangaza.
Amesema suala hilo la gharama katika ulingo wa sanaa, ndilo limechangia wasanii wengi kupenda kujiunga na lebo mbalimbali, huku kwa upande wake akisema hana mpango wa kujiunga katika lebo yoyote.
"Muziki wetu umefika mbali, kwa hiyo gharama za kurekod/video na kujitangaza ni kubwa hasa kwa mtu anayeanza, ndiyo maana sasa mtindo wa wasanii kuishi katika lebo unarudi, kwa upande wangu sina mpango wa kujiunga na lebo yoyote na sipendi". Amesema
Itazame hapa ngoma yake aliyokuja nayo akiwa na Peter Msechu