Thursday , 4th Jan , 2018

Mwanamuziki Nuru The Light ambaye aliwahi kutamba sana na ngoma ya 'Muhogo, andazi' amewataka mashabiki kuwakemea wasanii wanaofanya muziki wa kiki kwani kufanya hivo hakuwezi kufikisha mbali sanaa.

Akizungumza leo kwenye Planet Bongo leo wakati akitambulisha wimbo wake mpya alioupa jina Umeniacha amesema kwamba wasanii wanapaswa kutumia nafasi vizuri wanazopatiwa na siyo kuendekeza Kiki.

Nuru amesema kwamba licha ya kwamba vyombo vya habari vinasaidia kuu-push muziki kwa kuupa sapoti lakini hata mashabiki pia wanayo nafasi ya kuupeleka muziki mbali hata kwa kukemea.