Tuesday , 17th May , 2016

Mkongwe wa Bongo fleva Ambwene Yesaya AY kwa mara ya kwanza ameonesha meno yake ya thamani yenye asili ya madini ya silva na ice .

Msanii wa Bongo fleva AY

AY ameonesha kuwa yeye ni mmoja kati ya wasanii wenye fedha nyingi sana Bongo ingawa hakutaka kutaja thamani ya madini hayo katika meno yake kwa kuhofia usalama wake.

Pia kikawaida meno hayo tumezoea kuyaona tu kwa mastaa wenye fedha huko mbele wakiwa nayo kama vile Lily Wayne, Plies, Bird Man na wengineo yakifahamika kama grills.