
Banky W | Shaydee | Adasa
Uwezo mkubwa wa Banky W katika masuala ya usukaji video ndiyo yaliyouaminisha uongozi wa Empire Mates Entertainment, kumpa kazi kubwa kabisa ya kufanya video hiyo ya ngoma ya High ya Shaydee, akishirikiana na muongozaji mwenzake, Adasa.
Mitaa kwa sasa inasubiri kwa hamu kazi hiyo ya Shaydee, wakati huo Banky W akiendelea kufanya vizuri na video yake ya Lowkey, ambayo ameiongoza mwenyewe na kumtumia mwanadada Millen Magesse kutoka Tanzania kama 'modo' wake.