Thursday , 4th Aug , 2016

Baraza la Sanaa Tanzania BASATA limewataka washiriki wa Dance100% ambao wamefanikiwa kuendelea na nafasi ya robo fainali baada ya kushinda kwenye usaili kutambua kwamba ubunifu ndiyo msingi wa mafanikio katika kazi za sanaa.

Mkuu wa matukio ya sanaa kutoka BASATA Kurwijira N Maregesi alipokuwa akizungumza na washiriki wa Dance100%

Hayo yamesemwa na Mkuu wa matukio ya sanaa kutoka BASATA Bwn. Kurwijira N Maregesi alipokuwa akizungumza na washiriki ambao wamefaulu usaili wakati wakisaini mikataba ya ushiriki wao katika hatua muhimu zilizobakia.

''Ubunifu ndiyo msingi na mafanikio katika kazi za sanaa, hiyo ndiyo nguzo itakayokutofutisha wewe na msanii mwingine hivyo wakati mnajipanga kwa nafasi zinazoendelea jitahidini kuhakikisha kwamba ubunifu pamoja na nidhamu vitawafanya mfike mbali sana kupitia sanaa'' – Amesema Bwn. Maregesi.

Aidha amewataka washiriki hao kuthamini nafasi walizonazo na kutambua kwamba sanaa ni kazi kama kazi nyingine hivyo waiheshimu kazi hiyo pamoja na EATV ambayo imewezesha kuwaandalia nafasi hiyo ya kuonyesha vipaji vyao katika jamii.

Shindano la Dance100 linadhaminiwa na Vodacom kwa kushirikiana na Coca-Cola ambapo burudani ya aina yake inayooyeshwa na vijana kupitia shindano hilo inaonyeshwa na EATV pekee kila siku ya Jumapili saa moja jioni.

Tags: