
Msanii Diamond Platnumz
Mashabiki wengi wa Diamond Platnumz wamefurahishwa na jinsi msanii huyo alivyoweza kuchana vyema huku maneno yake ya kiswahili aliyoyatumia katika ngoma hiyo kuonesha kuwakosha wengi na kuwavuruga kabisa kwa furaha kutokana na midondoko yake kwenye 'remix' hiyo ambayo haijafahamika bado ataiachia lini.
"Moja ya mistari ya Diamond kwenye wimbo huo ni pamoja na "Hasa waambie dada zao Kariakoo waje Ulaya, wanajenga majungu mimi najenga vibanda, wanatisha visu kumbe mimi nina panga, mimi namuomba Mungu wanakesha kuwanga" Amesikika Diamond Platnumz akiimba
Baada ya kupost kipande hicho cha wimbo huo haya ni baadhi ya maoni ya mashabiki zake ambao wameonesha kufurahishwa na kipande cha 'remix' hiyo
"Diamond sasa jamani ananifanya nitetemeke mwili mzima anafanya vitu vya ajabu sana. Waambie na dada zenu waje Ulaya ha ha ha ha wamesikia" Shaibu Mgwaluv