Thursday , 13th Mar , 2014

Mwigizaji wa filamu wa kimataifa, Forest Whitaker, ametua huko Gulu nchini Uganda kwa ajili ya kuongeza uelewa kwa wenyeji juu ya umuhimu wa kujitolea na kushiriki katika shughuli za hisani ili kusaidia wale wenye uhitaji zaidi.

Forest ambaye kwa sasa anafanya vizuri kupitia filamu ya The Butler kati ya nyinginezo, katika ziara yake hii ya siku moja, ameweza kushiriki katika moja ya shughuli hizi za hisani, kusaidia wananchi wenye matatizo ya masikio ama usikivu.

Forest ambaye umaarufu wake huko Uganda zaidi unaletwa na ushiriki wake katika filamu ya The Last King of Scotland amekuwa ni moja kati ya wasanii wa filamu ambao mbali na kazi zao za uigizaji, wamekuwa na mchango mkubwa katika kusaidia jamii kwa kutumia uwezo na nafasi zao.