Monday , 10th Mar , 2014

Jimmy Gait, msanii wa muziki wa injili nchini Kenya baada ya kuzua gumzo kubwa na kazi yake mpya inayokwenda kwa jina Makekes kwa madai kuwa video hii haikuwa na maadili ya kidini kabisa, msanii huyu ameweka wazi kuwa kwa sasa yupo katika hara

Jimmy Gait amekiri kuwa, anafahamu kuwa bado kazi yake ya Makekes ambayo video yake imetoka mwezi uliopita inahitaji nafasi kutokana na upya wake, ila anaona umuhimu wa kuwa anatoa kazi mpya mara kwa mara kila inapowezekana.

Bado haijafahamika kama jitihada hizi za Jimmy Gait zina lengo la kuzima mjadala kuhusiana na kazi yake ya Makekes ambayo imepata maoni mbalimbali ya tofauti, ambapo kwa sasa kazi yake mpya aliyoahidi kutoa hivi karibuni tayari inangojewa kwa hamu na mashabiki na wadau mbalimbali wa muziki.