Antonie Semenyo
United inamtaja Semenyo kwa lengo la kuimarisha winga ya kushoto, eneo linaloonekana kuwa na changamoto kwa sasa. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ana kipengele cha kuachwa cha Pauni 65 milioni kinachoanza kutumika mwezi ujao.
Hatua hiyo mpango huo unaendana na mkakati mpya wa usajili wa Man United wa kuwalenga wachezaji waliothibitisha uwezo wao Ligi Kuu ya England. Semenyo amefunga mabao saba ya msimu huu, akivunja ukame wa miezi miwili katika sare ya mabao 4-4 dhidi ya United.
Kwa sasa hakuna mchezaji wa United aliyefunga mabao mengi ya ligi kuliko Semenyo, ambaye pia hayuko kwenye majukumu ya AFCON baada ya Ghana kushindwa kufuzu.
Semenyo anaweza kucheza pande zote za winga, lakini anaonekana kufaa zaidi upande wa kushoto, nafasi ambayo Dorgu ameshindwa kuifanya kuwa yake tangu asajiliwe.
