
Nay wa Mitego alipokutana na Waziri Mwakyembe, Dodoma
Hiyo ni baada ya Rais Magufuli kuamuru wimbo wake huo wa 'Wapo' ufunguliwe baada ya kufungiwa na BASATA huku akishauri ufanyiwe maboresho kwa kuongeza vionjo vipya.
"Nimeitikia wito wa Mhe. Waziri, nashukuru tumeongea mengi wanasema usikatae wito kataa maneno. Haikuwa kwa ubaya, hakuna cha kurekebisha kwenye wimbo wetu wa 'Wapo' ila aliyoyapendekeza Mh. Rais nitayafanyia kazi. Huu ni wimbo wenu mashabiki wangu wote Tanzania na duniani kote, 'Wapo' ujumbe umeanza kufika. Hakuna atakae badilisha mtazamo wangu". Aliandika msanii huyo
Pamoja na hayo Nay wa Mitego amesema anawategemea sana wananchi katika ulinzi wake kwa kuwa yeye hana 'Body-guard'
"Sina mlinzi wala Bodyguard nyie ndo walinzi wangu". Moja ya mstari aliyoandika Nay