Saturday , 30th Dec , 2017

Msanii wa filamu bongo aliyebarikiwa urembo wake ambaye pia kwa sasa ni mjasiriamali, Jackline Wolper, ameufahamisha umma kuwa hivi karibuni huenda akawekwa ndani na kuwa mke wa mtu, baada ya kutujulisha kuwa anatolewa mahari.

Kwenye ukurasa wake wa instagram Wolper ametoa taarifa ya kutolewa kwake mahari huku akimfikishia ujumbe Vanessa Mdee, kuwa ameshindwa kuhudhuria tukio la uzinduzi wa albam yake kwa kuwa yupo mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya tukio hilo.

"A very big Congratulations to my girl.. nimeskia umefanya kazi nzuri sana last night..Keep up the good work Girl Power... Nimeshindwa kuhudhuria si unajua niko Moshi kwenye tukio la mahari yangu, but nilitamani sana kuwepo, ila nitakuletea card ya mualiko wa harusi yangu tafadhali usikose, love you girl ", ameandika Jackline Wolper akimwambia Vanessa Mdee.

Baada ya hapo East Africa Television iliamua kumtafuta mlimbwende huyo atuthibitishie kama ni kweli au acount ilikuwa imedukuliwa, na kuthibitisha ni kweli yupo mkoani Kilimanjaro kwa tukio hilo.

"Ni kweli nimepost na kweli natolewa mahari, si unajua sisi Wachaga na mila zetu, kwa hiyo tupo huku, na mwanaume wangu kwanza sio Mtanzania hata Kiswahili chenyewe hajui, so nimeshamfundisha taratibu za kwetu", amesema Jackline Wolper.

Alichokiandika Jackline Wolper instagram