Friday , 16th Dec , 2016

Msanii wa muziki wa bongo fleva ambaye ni mkali kwenye miondoko ya RnB kutoka Wakali Kwanza, Makamua, leo ameweka wazi sababu ya wao kuachana na MJ Records na watu waliowatoa kwenye game.

Makamua

 

Akizungumza na East Africa Television, Makamua amesema wao kama wakali kwanza hawakuwa na mgogoro wowote na Mj Records na viongozi wao, lakini iliwapasa wasibakie Mj Records.

Hata hivyo kundi hilo limetangaza kurudi tena kwenye game, huku wakiwa na uongozi ule ule wa zamani wa Marco Chali na Mj Records.

Tazama video Makamua akizungumzia wao kutoka Mj Records.