Wednesday , 9th Jul , 2014

Msanii wa miondoko ya Bongo Fleva Izzo Bizness amewahakikishia mashabiki wake kuwa hivi sasa yeye ni moto wa kuotea mbali baada ya kuachia rasmi wimbo wake alioubatiza 'Walala hoi' ambao umetambulishwa leo rasmi.

Rapa Izzo Bisnezz

Izzo Bizness ameelezea kuwa hivi sasa anajipanga zaidi kuandaa kichupa cha wimbo huo ambao unalenga zaidi maisha ya watu walio katika hali duni kimaisha na amewasihi mashabiki wake wakae mkao wa kula kwa kichupa hicho kipya.

Pata kitu kipya kutoka kwake Izzo Bizzy 'Walala Hoi'.