Tuesday , 13th Nov , 2018

Mwanamuziki wa Hip Hop wa Marekani na muigizaji wa filamu, Jaden Smith, ameushtua ulimwengu baada ya kumtangaza hadharani mpenzi wake ambaye ni mwanaume mwenzie.

Msanii huyo ambaye ni mtoto wa pili wa msanii nguli wa Hollywood, Will Smith, ametoa taarifa hiyo masaa machache yaliyopita akiwa jukwaani akifanya show nchini Marekani, ambapo pia aliamua kumtaja rapper Tyler, the Creator kuwa ndiye mpenzi wake ingawa rapper huyo hataki watu wajue.

“Tyler, the Creator ni mpenzi wangu, ni kweli, yeye hataki tu kusema lakini Tyler ni mpenzi wangu, na amekuwa mpenzi wangu maisha yangu yote”, amesikika Jaden Smith.

Jaden hakuishia hapo aliendelea kuandika kwenye ukurasa wake wa twitter akimwambia boyfriend wake huyo, rapper Tyler The Creator, kuwa ameshaweka wazi sasa, hawezi kukataa.

Kutokana na hilo kumeibuka utata kuwa kama wawili hao wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja ama la, kutokana na Tyler kuonesha ishara ya kukataa kwa kichwa, wakati Jaden yupo jukwaani akitangaza uhusiano wao.

Kwa muda mrefu Jaden alikuwa akihisiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, baada ya kuonekana kuvaa mavazi ya kike kwenye matangazo ya nguo ya mbunifu mkubwa wa mavazi duniani, Louis Vuiton, jambo ambalo baba yake hakulifurahia

Rapper Tyler The Creator