
Lady Jay Dee ndani ya FNL
Akizindua wimbo huo katika kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na EATV, Lady Jay Dee amesema wimbo huo una mavunzo mazuri kwa jamii na kuwataka mashabiki na watu wote kuutafuta na kuusikiliza na kutazama video yake ili wafaidi ujumbe uliopo.
“Wimbo huu ujumbe wake ni tofauti na ule wa NdiNdiNdi kwa sababu NdiNdiNdi unafaa zaidi kupigwa kwenye kumbi za starehe, ila huu wa Sawa Na Wao ni wimbo ambao hata watu wazima wanaweza kuusikiliza na kupata ujumbe uliopo ndani yake” Amesema Lady Jay Dee
Amesema alichoamua kukionesha katika wimbo huo ni jinsi ambavyo baadhi ya watu hulazimika kuishi maisha yasiyo ya kwao, ili kufanana na kundi fulani la watu kwa lengo fulani, ambapo hufikia hatua ya kuigiza maisha yasiyo halisi.
Akitolea mfano mwanadada anayeonekana katika video hiyo, ambaye ameonekana akipaka rangi viatu vyake ili vionekane vya gharama kubwa kama walivyonavyo wenzake, Jay Dee amesema kuwa hayo ni mambo ambayo hutoke katika maisha ya kawaida, ambapo watu wengi hujikuta wakiumia nafsi kwa kushindwa kumudu gharama kubwa za mavazi kwa lengo la kufanana na watu wengine wenye uwezo mkubwa mkubwa.
Amesema ni vizuri mtu anapokuwa kwenye kundi fulani la watu akajaribu kufanana nao ili kuwa sawa na wao.
Aidha Lady Jay Dee amewashukuru mashabiki wake kwa namna wanavyoendelea kumuunga mkono katika kazi zake za sanaa na ameahidi kuendelea kuwapa vionjo tofauti na ujumbe wenye mafundisho katika jamiii.